Winga wa kimataifa wa Ivory Coast Gervinho na klabu ya Arsenal yuko kwenye hatua za mwisho za kuihama klabu hiyo ambapo anakaribia kujiunga na As Roma ya Italia .
Gervinho
tayari amefikia makubaliano binafsi na klabu hiyo huku Roma na Arsenal
zikiwa kwenye hatua za mwisho za mazungumzo ya bei ya mchezaji huyo .
Gervinho
alijiunga na Arsenal misimu miwili iliyopita akitokea Lille Metropole
ya Ufaransa lakini ameshindwa kupata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha
kwanza kwa muda wote aliokuwa na klabu hiyo ya London.
Kwa muda mrefu mchezaji
huyo amejikuta akishindwa kuwa kipenzi cha mashabiki wa Arsenal kutokana
na kuwa anakosa mabao mengi ya wazi awapo uwanjani hali inayofanya
mashabiki kumzomea mara nyingi . Cha Kushangaza kuhusu Gervinho ni
kwamba amekuwa akicheza vizuri akiwa na timu ya taifa na hata kufunga
mabao muhimu tofauti na anapokuwa na Arsenal
|
No comments:
Post a Comment