Kocha mpya wa klabu ya Barcelona Gerardo Tata Martino ametoa tamko juu ya mustakabali wa kiungo wa klabu hiyo Cesc Fabregas .
Tata amesema kuwa
uamuzi wa kubaki ama kuihama klabu ya Barcelona upo mikononi mwa
mchezaji mwenyewe na hawezi kumuingilia katika uamuzi wowote
atakaoufanya .
Kocha
huyo ameongeza kuwa anaamini kuwa Cesc anaipenda Barca na hataondoka
kwenye klabu hiyo baada ya kuwepo kwa ofa za kumsajili toka klabu ya
Manchester United.
Cesc
alikuwa uwanjani hapo jana wakati Barca ilipocheza na Santos katika
mchezo wa kirafiki ambapo mabingwa hao wa zamani wa ulaya walishinda kwa
mabao nane bila huku Cesc akifunga mabao mawili .
Manchester United
walipeleka ofa mbili kwa ajili ya kiungo huyu ambapo ya kwanza ilikuwa
paundi milioni 26 kabla ya kuja na ya pili ambayo iliongezeka na
kufikia paundi milioni 31 . United huenda wakarudi na ofa ya tatu ambayo
itakuwa ya mwisho ambayo inaaminika kuwa itafikia paundi milioni 41.
|
No comments:
Post a Comment