Kocha Mhispania Pep Guardiola ameiongoza Bayern Munich kutwaa taji
lake la kwanza kwa msimu huu baada ya kuifunga Chelsea kwa mikwaju ya
penati na kutwaa ubingwa wa UEFA Super Cup.
Chelsea ndio walioanza kupata bao mapema kwenye dakika ya nane
mfungaji akiwa Fernando Torres ambaye alifunga kwa shuti akipokea krossi
ya Mjerumani Andre Schurrle.
Bayern Munich walisawazisha bao hilo kitia kwa Frank Ribery ambaye
alikosa nafasi nyingi za wazi kabla ya kufunga bao hilo mwanzoni mwa
kipindi cha Pili.
Mchezo huo uliliazimikankwenda kwenye muda wa nyongeza baada ya
dakika tisini kumalizika huku timu zote zikiwa zimefungana bao 1-1 .
Chelsea walipata bao mwanzoni mwa kipindi cha kwanza cha muda wa
nyongeza mfungaji akiwa Edin Hazard ambaye alipiga shuti lililomzidi
kipa wa Bayern Manuel Neur.
Bayern Munich hawakukata tamaa na waliendlea kushambulia na
mashambulizi hayo yalizaa matunda mwishoni mwa dakika za nyongeza wakati
kiungo Javi Martinez alipofunga bao la kusawazisha .
Mshambuliaji Romelu Lukaku alishuhudia penati yake ikiokolewa na kipa
wa Bayern Neur na kuipa timu hiyo ya Ujerumani ushindi wa penati 5-4. |
No comments:
Post a Comment