Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kampuni ya Azam Media leo
(Agosti 30 mwaka huu) wamesaini mkataba wa haki za kipekee za
televisheni (exclusive rights) utakaoiwezesha Azam TV kuonesha mechi za
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
Mkataba huo wa miaka mitatu wenye
thamani y ash. 5,560,800,000 umesainiwa kwenye hoteli ya Serena jijini
Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Athuman Nyamlani amesaini kwa niaba ya
TFF wakati aliyesaini kwa upande wa Azam Media ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa
kampuni hiyo Thys Torrington.
Ligi Kuu ya Tanzania sasa itakuwa ikipatikana kupitia kisimbuzi
(decorder) cha Azam TV kitakachokuwa na chaneli zaidi ya 50. Mechi hizo
zinatarajiwa kuoneshwa moja kwa moja wakati wowote kuanzia mwezi ujao.
Makamu wa Rais wa TFF, Nyamlani amesema udhamini huo wa televisheni ni
fursa pana kwa klabu kwani zitaweza kujitangaza zaidi huku wachezaji
nao wakipata soko zaidi za mpira wa miguu.


No comments:
Post a Comment