Manchester City nao watalazimika kupepetana na bingwa wa kombe hilo
la klabu bingwa ,Ulaya Bayern Munich, CSKA Moscow na Viktoria Plzen.
Wapenzi wengi wa soka wanajiuliza je safari hii baada ya kupata kocha
mpya mwenye uzoefu katika michuano hiyo ya kombe la klabu bingwa Manuel
Pellegrini,Man City wataweza kupiga hatua na kuingia katika mechi za
muondoano?
Kwa upande mwengine Kocha mpya wa Manchester
United ,David Moyes hatakuwa na kazi kubwa sana kwani watapepetana na
Shakhtar Donetsk, Bayer Leverkusen ya Ujerumani na Real Sociedad ya
Uhispania.
Miongoni mwa timu za Uingereza ni Chelsea peke
yake ndio yenye kazi nyepesi kwani katika kundi lao watamenyana na
Schalke ya Ujerumani, FC Basel na Steaua Bucharest.
Mechi za kwanza za makundi zinapaswa kugaragawa kati ya Septemba17-18 mwaka huu. |
No comments:
Post a Comment