Meseret Defar wa Ethiopia amedhihirisha umaarufu wake
katika mbio za kina dada za mita elfu tano pale alipomshinda Muethiopia
mwenzake Tirunesh Dibaba wakati wa mashindano ya IAAF Diamond league
zilizofanyika mjini Zurich.
Meseret Defar alizitimuka mbio hizo kwa muda wa
dakika 14:32.83, akifuatwa na Dibaba na Mkenya Mercy Cherono, ambaye ni
mshindi wa medali ya fedha katika mashindano ya dunia.
Katika
mbio za mita elfu moja mia tano kwa wanaume, bingwa wa dunia Asbel
Kiprop, alimaliza katika nafasi ya sita, huku mkenya mwezake Silas
Kiplagat akiibuka na ushindi.
Ayanleh Souleiman wa Djiobouti akiridhika na nafasi ya pili akifuatwa na Nixon Chepseba.
Bingwa wa dunia wa mbio za mita mia nane kwa
kina dada, Euinice Sum kwa mara nyingine tena aliwapiku wapinzani wake
katika mbio na kudhihirisha umaarufu wake katika mbio hizo.
Sum alitumia muda wa dakika moja sekunde 58
nukta 82 naye bingwa wa zamani wa dunia Mariya Savinova wa Urussi
akimaliza katika nafasi ya pili akifuatwa na Malika Akkoui. |
No comments:
Post a Comment