Kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas hatimaye amevunja ukimya kuhusu suala la Manchester United kutaka kumsajili kwa kusema anataka kubaki nchini Spain.
Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal akiongea kwenye mkutano wa waandishi wa habari jijini Kuala
Lumpur mahala ambapo Barcelona wapo kwa ajili ya maadalizi ya msimu mpya.
Fabregas
alisema: 'Ndoto yangu siku zote imekuwa kuichezea Barcelona na hakuna
kilichobadilika. Nina furaha sana kuwa hapa na sijawahi kufikiria kuhusu
kuondoka.
"Sijawahi kuwa na shaka juu hilo. Haijanigharimu chochote kurudi Barcelona na sasa nataka kuwa mshindi nikiwa hapa.
'Ni
heshima kubwa kwa Manchester United kuleta ofa mbili kwa ajili yangu,
lakini hakujawahi kuwa na mazungumzo. Sijawahi kuongea na klabu yoyote
tangu nimejiunga na Barcelona miaka miwili iliyopita.
'Siku zote nimekuwa nikitambua ninavyothaminiwa na klabu. Kila mut ameniambia namna anavyonitegemea, sijwahi kupata ishara yoyote tofauti ya kuhisi sihitajiki.
'Sikutaka
kusema lolote huko mwanzo kwa sababu kwangu mimi kila kitu kilikuwa
wazi kwamba nilikuwa nataka kuendelea kubaki hapa. Niliiambia klabu
nitaongea itakapofika zamu yangu.
'Kuna baadhi ya vitu vilitengenezwa, lakini havikuwa vya kweli - hasa la kusema kwamba nimeomba kuongezewa mkataba,' alisisitiza Cesc Fabregas |
No comments:
Post a Comment