PSI

PSI

Thursday, August 8, 2013

Umeyasikia ya Rooney na kocha wake.

Kocha wa United David Moyes hii leo alilazimika kumuamuru mshambuliaji Wayne Rooney kufanya mazoezi na kikosi cha vijana cha timu hiyo baada ya mshambuliaji huyo kuendelea kushikilia uamuzi wa kutaka kuihama Man United .
Rooney amekuwa akilazimisha kuuzwa kwenda klabu ya Chelsea huku kocha wake David Moyes akishikilia uamuzi wa kutomuuza mchezaji huyo . 
Tukio hili ambalo lina filamu inayofanana na ile inayoendelea kwenye klabu ya Liverpool baina ya kocha Brendan Rogers na mshambuliaji Luis Suarez limechukua sura mpya baada ya mshambuliaji huyo kuachwa nyumbani wake wenzie walipopanda ndege kwenda Sweden kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya AIK Stokholm ambapo United ilitoka sare na klabu hiyo .

Rooney aliachwa nyumbani huku mashabiki wa United wakitaarifiwa kuwa mshambuliaji huyo ana jeraha la bega ambalo litamuweka nje kwa muda usiopungua wiki moja 
Kwa muda wa takribani miezi miwili sasa ulimwengu wa soka umekuwa ukijazwa na tetesi zinazohusu uhusiano wa Wayne Rooney na klabu yake , uhusiano ambao unazidi kuharibika kila siku.

Hadi sasa picha halisi inaonekana kuwa mshambuliaji huyo amegundua kuwa hana nafasi kwenye kikosi cha kwanza hali inayomfanya atake kuhama na kwenda mahali ambako atakuwa na nafasi ya kudumu .
Taarifa za ndani toka Old Trafford zinasema kuwa baadhi ya wachezaji wa United wameanza kukerwa na taarifa na hizi na wameridhia kuondoka kwa mchezaji huyo kutokana na kuchoshwa na ubinafsi wake .
Rooney amekuwa akitakiwa na klabu ya Chelsea huku United ikisita kumuuza kwenda klabu hiyo kwa kile ambacho inahofia kumuimarisha adui huku ikipungukiwa na silaha muhimu .


No comments: