Usajili wa wachezaji mbalimbali unazidi kushika kasi barani ulaya.
Winga Mshambuliaji wa Ivory Coast,Gervais Lombe
Yao Kouassi maarufu kama Gervinho amekamilisha uhamisho wa kuichezea As
Roma ya Italia.
Uhamisho huo wa Gervinho umetajwa kuwa wa pound milioni 8 walizopewa Arsenal.
Gervinho alihamia Arsenal mwaka 2011 akitokea Lile ya Ufaransa.
Msimu wake wa kwanza aliifungia Arsenal magoli manne kabla ya kufunga magoli saba msimu uliopita.
Amekuwa akipata ushindani wa kuwemo kwenye
kikosi cha kwanza cha Arsene Wenger, na huenda usajili wake wa kuhamia
Seria A utakuwa changamoto mpya kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka
26. |
No comments:
Post a Comment