Jose Mourinho amesisitiza kwamba atapigana mpaka siku ya mwisho katika jaribio lake la kumsaini Wayne Rooney.
Chelsea
tayari walishatuma ofa mbili ambazo zimekataliwa na Manchester United,
ofa ya mwisho inayotajwa kuwa ni zaidi ya paundi million 25 ilitumwa
jumapili. Lakini Mourinho alisema: "Hatuna kizuizi cha muda kwenye suala
hili.
‘Tumemuona
Rooney kama ni mchezaji ambaye tungependa kuwa nae. Tumefanya kila kitu
katika utaratibu unaopaswa na tutafanya hivyo mpaka siku ya mwisho ya
usajili. Tunafnya kila kitu tukizingatia sheria, kutoa ofa rasmi kwa
klabu moja kwa moja.
‘Hakujawahi kuwepo kwa mawasiliano na mchezaji, hakijatokea kitu kama hicho. Tusubiri tuone kama mambo yatabadilika.’
Rooney
inaaminika kwamba amemwambia kocha wake David Moyes kwamba anataka
kuondoka, lakini United imekuwa ikisisitiza kwamba hauzwi.
|
No comments:
Post a Comment