Luis
Suarez amezidi kupata vizingiti vikubwa katika harakati zake za kutaka
kuhama Liverpool, baada ya kuambiwa na mmiliki wa Liverpool John Henry
warning: “Huendi popote”.
Mmiliki huyo wa Liverpool amesema
kwamba ni upumbuvu kuanza hata kufikiri kufanya biashara na Arsena ya
mshambuliaji huyo wa Uruguay. Na mmarekani huyo amesema kwamba
kitendo alichokifanya Suarez kilivuka mipaka, huku akisisitiza kwamba
mshambuliaji huyo hatouzwa kwenda klabu yoyote mpaka dirisha la usajili
litakapofungwa September 2 - pia akisema uamuzi wa kutokumuuza Surez
hautokani na masuala ya fedha. Henry alisema: “Hatuwezi kumuuza Luis. Ni
kwa sababu za kisoka kabisa, na sio masuala ya fedha.
“Hii ni
kwasababu mpaka sasa ni vigumu kupata mchezaji wa kuziba pengo lake kwa
maana wachezaji wazuri wote wameshahama. Hivyo ni sababu za kisoka,
hatuwezi kumuuza - hasa kwa klabu ya Arsenal.
“Kuwauzia mahasimu wetu mchezaji huyu utakuwa ni upumbavu kabisa." |
No comments:
Post a Comment