![]() |
| Kocha wa Manchester United David Moyes August 11 2013 ameanza
rasmi kazi yake kama kocha wa timu hiyo kwenye mechi ya ushindani baada
ya kuiongoza timu hiyo kupata ushindi wa mbili bila kwenye mechi ya
kuwania ngao ya jamii dhidi ya Wigan Athletic. United ilipata magoli yake kupitia kwa mfungaji bora wa ligi kuu ya England kwa msimu uliopita Robin Van Persie ambae ndio alifunga hizo goli zote mbili ambapo club hii iliyoanza kuitwa Manchester United mwaka 1902 iliingia kwenye hii mechi bila mkali wao Wayne Rooney ambae hakuchaguliwa kwa sababu ni majeruhi. Pamoja na hiyo sababu ya majeraha yake, bado ishu ya Rooney ndani ya Manchester United ni kama kitendawili. Unaambiwa Manchester United ndio club ya kwanza England kushinda European Cup mwaka 1968 chini ya management ya Matt Busby. |
![]() |
Ulimis kuhusu mechi ya Manchester United August 11 2013?United ilipata magoli yake kupitia kwa mfungaji bora wa ligi kuu ya England kwa msimu uliopita Robin Van Persie ambae ndio alifunga hizo goli zote mbili ambapo club hii iliyoanza kuitwa Manchester United mwaka 1902 iliingia kwenye hii mechi bila mkali wao Wayne Rooney ambae hakuchaguliwa kwa sababu ni majeruhi. Pamoja na hiyo sababu ya majeraha yake, bado ishu ya Rooney ndani ya Manchester United ni kama kitendawili. Unaambiwa Manchester United ndio club ya kwanza England kushinda European Cup mwaka 1968 chini ya management ya Matt Busby.
Beki wa Manchester United ambae pia ni nahodha msaidizi wa timu hiyo
Mfaransa Patrice Evra, alikuwa mchezaji bora wa mchezo huo baada ya
kucheza kwa kiwango cha juu kwa kuchangia kwenye ufungaji wa goli zote
mbili.
Taji la ngao ya Jamii linakuwa taji la kwanza kwa kocha mpya David
Moyes tangu alipoteuliwa kurithi nafasi ya kocha wa zamani Sir Alex
Ferguson mwishoni mwa msimu wa ligi uliokwisha ambapo Moyes ataanza
rasmi kampeni ya utetezi wa ubingwa wa ligi kuu ya England kwa klabu
yake wiki ijayo wakati Manchester United watakapokutana na Swansea City
kwenye mechi ya kwanza ya ligi.
|


No comments:
Post a Comment