Chelsea imepataushindi wake wa kwanza kwenye Champions league msimu huu
ikiibuka na ushindi wa mabao 0-4 dhidi ya wenyeji wao Steaua Bucharest
Ramires akiingia wavuni mara mbili,Lampard mara moja na bao lingine
Steaua wakijifunga wenyewe kufuatia mkwaju uliopigwa na Samuel Etoo.
Arsenal nao si haba wamepata ushindi wao wa pili kwenye chyampions
league wakiichapa Napoli ya Rafa Benitez mabao 2-0 huku Mesut Ozil
akianza kutumbukia wavuni.
Barcelona wakapata ushindi wa bao 1-0 kwa taabu huko Celtic Park mbele
ya wenyeji wao Celtic ambao walilazimika kubaki kumi baada ya mchezaji
wao mmoja kutolewa kwa kadi nyekundu.
Mario Balotelli akaibeba AC Milan isiaibike mbele ya Ajax baada ya
kutupia wavuni penati iliyopatikana dakika za mwisho na mchezo
kumalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.










No comments:
Post a Comment