Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limewasilisha rasmi
suala la madai ya aliyekuwa Kocha wa Yanga, Kostadin Papic dhidi ya
klabu hiyo katika Kamati ya Hadhi ya Wachezaji.
FIFA imesema imepeleka rasmi suala hilo katika kamati yake hiyo baada ya kupokea vielelezo vya Papic anayedai kuidai Yanga dola 10,000 za Marekani pamoja na vile vya Yanga inayodai kumlipa kocha huyo fedha zote alizokuwa akiidai klabu hiyo.

Kwa taratibu za FIFA, hivi sasa haitapokea vielelezo vingine kutoka
pande hizo mbili, na badala yake Kamati hiyo inayoongozwa na Theo
Zwanziger kutoka Ujerumani itafanya uamuzi na kuziarifu pande husika.
Zwanziger kitaaluma ni mwanasheria.
Papic aliyeinoa Yanga kwa vipindi viwili tofauti aliwasilisha malalamiko
yake FIFA akidai hadi mkataba wake unamalizika klabu hiyo ilikuwa
haijamlipa dola 10,000 za Marekani.

No comments:
Post a Comment