Inatokana na mshambuliaji huyu sasa hivi kuruhusiwa na mamlaka kuu za
soka duniani (FIFA) kuchezea club yake ya zamani ya Villa ya Uganda
wakati ambao bado club yake ya Simba haijalipwa hata shilingi moja na
waarabu hao wa Tunisia.
Mamlaka husika za soka Uganda zilipambana kwa faida ya mchezaji na
taifa la Uganda kuhakikisha mshambuliaji huyu hakai bure baada ya
kurejea kwa kile alichokisema kwamba ni kulimbikizwa mishahara yake kwa
muda mrefu bila malipo.
TMS manager wa shirikisho la soka Tanzania TFF Saad Kawemba
amezungumza kuhusu ushiriki wao kama shirikisho kuzisaidia club za
Tanzania hasahasa hii ishu ya Simba kushindwa kupata haki yao juu ya
mauzo ya Okwi na kusema ‘tayari nimeona Simba wameandika barua na sisi
tutaipitisha iende moja kwa moja kwenye player status committee
ili waione hiyo kesi, hizo ndio documents ambazo zinakwenda zikisema
hawa watu waliahidi kufanya hivi na hawajafanya hivyo tunaomba sasa
walazimishwe kufanya hivi’
‘Kiukweli kabisa tunahitaji kuwa wavumilivu nadhani watu wanaweza
kudhani kiongozi flani kafanya hivi, kakosea kachukua kitu flani na
nini…… hapana, kwa sababu katika transfer inaonekana kwenye system wale
hawajalipa, nizungumze jambo moja ambalo liko wazi kwenye system ni
kwamba pale club mbili zinapokubaliana kuuziana mchezaji, mchezaji
anaruhusiwa kwenda kwenye club mliyokubaliana na malipo yatafata baadae,
kutokuwepo kwa malipo hakumzuii mchezaji kuhama… hiyo ni kanuni ya
kwanza ya uhamisho’ – Kawemba
‘Kwa faida ya watu wote ni kwamba sisi hapa nyumbani tumezoea kabisa
mchezaji hawezi kutoka mpaka nilipwe lakini kwenye mpira duniani ni
kwamba mnakubaliana alafu pesa zinalipwa kidogokidogo, tunaomba watu
wawe wavumilivu kwasababu tayari kesi iko mikononi mwa FIFA walikua nayo
toka mwanzoni wakaomba Simba waongee na Tunisia na kweli walikwenda na
kukubaliana ila hayajatekelezwa’ – hayo ni maneno ya Kawemba akiongea na
sports Extra ya Clouds FM.
‘Kesi ya Simba iko wazi kabisa mbele ya FIFA na tunaamini kabisa
kwamba Simba watanufaika na kesi hiyo kwa sababu hawajafanya kosa lolote
kwenye uhamisho huo, nguvu yetu ni kuhakikisha kesi hii tunaishinda na
club yetu inapata haki yake’ hii ni sentensi nyingine ya Kawemba
unaeweza kumsikiliza hapa chini pia
No comments:
Post a Comment