Walcott akiondolewa nje ya uwanja baada ya kupata jeraha
Arsenal imepata pigo baada ya
mchezaji wake Theo Walcott kuthibitishwa kuwa atakosa kushiriki michuano
ya Kombe la dunia kwa kuwa atakuwa kando kwa takriban miezi sita baada
ya kupata jeraha la mguu.
mshambuliaji huyu wa Uingereza mwenye umri wa
miaka 24 alipata jeraha wakati wa michuano ya Kombe la FA siku ya
jumamosi walipokutana na Tottenham na kuichapa mabao 2-0.Michuano ya Kombe la dunia inatarajiwa kuanza tarehe 12 mwezi Juni, huku Uingereza ikitarajiwa kukipiga na Italia katika mchezo wake wa kwanza siku mbili baadae.
Rekodi ya Walcott akiwa na Kikosi cha Uingereza.
-Alionekana kwa mara ya kwanza na kikosi cha Uingereza mwaka 2006 ilipocheza na Hungary.
-Alisisimua wengi baada ya kuwa katika kikosi hicho kwenye Kombe la dunia mwaka 2006 akiwa na umri wa miaka 17 kabla ya kuingia kwenye ligi kuu nchini Uingereza.
-Aliwahi kufunga mabao matatu dhidi ya Croatia mwezi Septemba mwaka 2008.
-Katika hatua ya kushangaza aliachwa katika kikosi kilichocheza michuano ya kombe la dunia mwaka 2010 nchini Afrika kusini.
Walcott alichukuliwa kutoka Southampton mwaka 2006 kwa kititta cha Pauni milioni 12.5.
No comments:
Post a Comment