Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba na
Zambia Felix Muamba Sunzu leo amerudi dimbani kuitumikia tena klabu yake
ya Simba na kuifungia goli la pekee na la ushindi kwenye mchezo wa
kombe la Urafiki linaloshindaniwa huko Zanzibar.
Simba imeifunga timu ya vijana ya Zanzibar Karume Boys kwa bao 1-0 liliowekwa kimiani na Mzambia huyo.
Kwa matokeo hayo Simba ambao walianza vyema michuano hiyo
inayofanyika kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa kwa ushindi wa magoli 2-0
dhidi ya mabingwa wa Zanzibar, Mafunzo kabla ya kuja kushikiliwa kwa
sare ya 1-1 na Azam, ambao ni washindi wa pili wa Ligi Kuu ya Bara.
Azam FC ilimaliza ikiwa ya pili kwa kuwa na pointi 5 baada ya sare mbili na ushindi katika mechi iliyochezwa mapema jana.
Katika mechi hiyo, Azam iliilaza Mafunzo ya hapa kwa mabao 3-2.
|
No comments:
Post a Comment