Kwa mara ya pili kwenye maisha yake ya
soka - kocha mkongwe Luis Van Gaal hatimaye amepata nafasi ya
kusahihisha makosa yake aliyoyafanya miaka sita iliyopita kwa kuiongoza
Uholanzi kukosa nafasi ya kucheza kwenye kombe ladunia kwa mara ya
kwanza.
Siku kadhaa baada ya kocha Bert van
Marwijk kujiuzulu kuifundisha Uholanzi baada ya kucheza kwa kiwango
kibovu kwenye Euro 2012, leo hii amepata mrithi wake - Luis van Gaal.
Van Gaal kocha wa zamani wa Ajax,
Barcelona na Bayern Munich anamrithi Bert, huku ikiwa ni kipindi chake
cha pili kuiongoza Holland.
Baada ya kutambulishwa kwa waandishi wa
habari Van Gaal alisema: "Ni changamoto niliyokuwa nikiisubiri sana,
nashukuru nina nafasi ya kurekebisha palipoenda vibaya mara mwisho
nilivyokuwa mwalaimu wa timu ya taifa."
Kocha huyu mwenye miaka 60 amesaini mkataba wa ambao utampeleka mpaka kwenye fainali za kombe la dunia 2014.
|
No comments:
Post a Comment