PSI

PSI

Friday, July 6, 2012

KWANINI IKER CASILLAS ANASTAHILI KUSHINDA TUZO YA UCHEZAJI BORA WA DUNIA

Mjadala ulishaanza. Huku Spain wakisherehekea ushindi wao wanusu fainali  dhidi ya Ureno kwenye Euro 2012, mjadala ukawa ukageukia kwenye tuzo ya Ballon d'Or.  Cristiano Ronaldo alicheza kikubwa cha kutosha kwenye michuano hiyo kiasi cha kumfanya achukue tuzo ya uchezaji bora wa dunia? Au itakuwa Lionel Messi kwa mara ya nne mfululizo?

Usiku uliofuatia, Andrea Pirlo alionyesha kiwango cha hatari na kuiongoza Italy kupata ushindi wa usiotegemewa dhidi ya Ujerumani kwenye hatua ya nusu fainali. Na baada ya fainali, Kiungo wa Spain Andres Iniesta akaingia kwenye mchuano wa tuzo hiyo baada ya kuiongoza La Roja kutoa kipigo cha mbwa mwizi kwa Italia huku akimfunika Andrea Pirlo.

Lakini vipi kuhusu mwanaume aliyebeba kombe la Euro kwa Spain jumapili iliyopita?

Iker Casillas ndio jina jipya ambalo limeibuka katika mchuano huu wa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa FIFA. Akiwa amepewa sifa na Pele huku Di Stefano akimuondoa - mawazo tofauti yameshaanza kujitokeza.

Golikipa huyo wa Spain aliiongoza La Roja kupata ushindi mkubwa michuano hiyo iliyofanyika Oland na Ukraine, akiweka rekodi mbalimbali ambazo hakuna magolikipa wengine duniani wamewahi kuzifikia.

Jaokuwa timu yake mara nyingi imekuwa ikitawala mpira, lakini pale anapohitajika kuzuia mashambulizi hufanya hivyo kwa usahihi mkubwa. Kipa huyo mwenye miaka 31, aliokoa vizuri sana mpira uliopigwa na Ivan Rakitic wakati mchezo ukiwa 0-0 dhidi ya Croatia - goli ambalo kama wangefungwa lingeweza kuwaondoa kwenye michuano hiyo mabingwa hao kwenye hatua ya makundi. Pia kuokoa mkwaju wa penati ya Joao Moutinho uliwazuia kuwapa uongozi Ureno kwenye hatua ya penati na kuwapa nguvu zaidi baada ya Xabi Alonso kukosa penati yake ya kwanza kwa Spain iliyokolewa na Rui Patricio.

Kwenye fainali, Iker aliokoa michomo kadhaa ya hatari iliyoelekezwa golini kwake, wakati Spain wakiongoza kwa 2-0, kabla ya mchezo kuendelea na kuisha kwa Italy kufungwa 4-0.

Mechi hiyo ilikuwa ya 137 kwa Ikerkuichezea Spain na sasa amebakisha mechi 11 kumfikia golikipa Andoni Zubizarreta. Lakini kubwa zaidi mafanikio ya kwenye mchezo huo wa fainali - ulimfanya golikipa huyo wa Madrid kuwa mchezaji wa kwanza kushinda mechi 100 kwenye level ya kimataifa. Alivunja rekodi ya Dino Zoff ya kucheza dakika 494 bila kufungwa goli kwenye Euro, huku Casillas akicheza dakika 511 bila kufungwa goli - Antonio Di Natale alikuwa ndio mshambuliaji wa mwisho  kumfunga Iker.

Pia Saint Casillas alikuwa na msimu mzuri sana na Real Madrid, akikumbukwa zaidi kwa kuiongoza Blancos kuifunga Barca 2-1 huku akiokoa mpira muhimu wa Xavi mwezi wa nne pale Nou Camp.

Casillas akiwa kiongozi wa timu chini Jose Mourinho waliongoza Los Blancos kubeba kombe la kwanza la La Liga  tangu mwaka 2008.

Mchezaji mwenzie wa Madrid, Cristiano Ronaldoanaweza akawa ndio mtu aliyechangia zaidi mafanikio ya Madrid, lakini kushindwa kwake kuiongoza Ureno vizuri dhidi ya Spain kwenye Euro 2012 kunaweza kumuangusha, wakati Messi akishinda kombe moja tu dogo la mfalme huku akivunja rekodi ya mabao ulaya kwa kufunga mabao 73 lakini pia akakosa  kushinda kombe muhimu la La Liga - huku akiwa hajacheza michuano ya mashindano ya kimataifa. Performance ya Pirlo pia haikutosha, baada ya Spian kuwaaibisha waitaliano mjini Kiev jumapili iliyopita, kwa maana mchezaji mmoja wa La Roja anastahili kubeba tuzo hiyo.

Xavi na Iniesta wamecheza vizuri na kiukweli wanastahili kuwemo kwenye mchuano, lakini ukiangalia kimafanikio Casillas anastahili kuchukua tuzo hii ya Ballon d'Or.

No comments: