Hatimaye siku mbili baada ya kutua
nchini kocha Tom Saintifiet kutoka nchini Ubelgiji, leo ameingia
mkataba wa kuifundisha klabu ya Yanga
kwa kipindi cha miaka miwili.
Akizungumza mara baada
ya kuingia mkataba huo katika Makao Makuu ya klabu ya Yanga , Mwalimu huyo
amesema anatarajia kufanya kazi kwa nguvu sana ili kuhakikisha Yanga inafanikiwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania
Saintifiet
amesema Mkataba huo wa miaka miwili amesema anatarajia kuutumia katika
kuleta maendeleo katika Klabu ya Yanga ikiwemo kukuza vipaji katika
soka la Vijana.
Naye Katibu Mkuu wa klabu ya
Yanga, Mwesiga Selestine amesema Mkataba huo huenda ukawa ni endelevu
iwapo uongozi utaridhishwa na mwenendo wa Kocha huyo.
|
No comments:
Post a Comment