Kipa wa Barcelona Victor Valdes amesema
amecheza na wachezaji wote wawili Ronaldinho na Lionel Messi lakini kwa
asilimia 100 anaamini Gaucho alikuwa mchezaji mwenye kipaji kikubwa
kuliko wote ambao amewahi kuwashuhudia akiwemo Messi. Kipa huyo mwenye
miaka 30, aliiambia Terra TV.
Akiwa anatajwa sana kama mmoja ya wachezaji bora kabisa kuwahi kutokea
ulimwenguni, Messi ameuwasha moto kwenye La Liga katika kipindi cha
miaka 8, akivunja rekodi mbalimbali ikiwemo ya kufunga mabao mengi.
Lakini, Valdes anaamini Ronaldinho kipekee zaidi aliibadilisha historia
ya Barca alipowasili Nou Camp 2003, na kuchangia kwa mafanikio
wanayoyapata kikosi cha sasa.
"Siku zote nimekuwa nikisema kwamba Rony aliibadilisha historia ya klabu
alipokuwa akicheza hapa. Alikuwa kiongozi wa timu ambayo ilibadilisha
histori yetu.
"Hatukuwa tumeshinda taji lolote kwa miaka mingi. Alikuja na kuifanya
Barca kuwa na nguvu na kuifanya kuwa klabu kubwa inayojulikana duniani
kote kwa uwezo wake. Namshukuru sana kwa hilo. Naweza kusema ndio
mchezaji mwenye kipaji kikubwa kuliko wote ambaye nimewahi kushea nae
chumba cha kubadilishia nguo. Alikuwa anafanya vitu vyake vya
kustajaabisha kila siku.
|
No comments:
Post a Comment