Apparently utamu wa Pepsi umemkosesha
dili lenye thamani ya zaidi ya Billioni 2 za kibongo mchezaji wa
kimataifa wa Brazil Ronaldinho Gaucho baada ya kampuni ya Coca-Cola
kumpiga chini kwenye kazi ya ubalozi baada ya kuonekana akitumia
kinywaji cha wapinzani wao kibiashara.
Mchezaji huyo wa zamani wa
Barcelona alikuwa akiwahesabu Coca-Cola kama moja ya makampuni mengi
anayofanya nayo kazi kwa kumdhamini, lakini akufanya kosa la kuonekana
akinywa kinywaji cha Pepsi wakati wa mkutano wa waandishi wa habari.
Kiwango
cha Ronaldinho tangu arudi Brazil na ugomvi wake na klabu ya Flamengo
umekuwa ukimfanya atengeneze sana vichwa vya habari vya magazeti kwa
kipindi cha miezi kadhaa iliyopita.
Na kufuatia kwa kosa lake la
hivi karibuni, Coke hawakuonyesha kusita katika kuukatisha mkataba wao
na kiungo huyu mwenye miaka 32 na mchezaji bora wa dunia wa zamani wa
FIFA.
"Kitendo cha kuonekana akinywa Pepsi kimeharibu taswira
yake mbele ya wanywaji wa Coke. Watamuelewa vipi balozi anayewatangazia
bidhaa hi halafu yeye anatumia nyingine. Kwa hili tumeamua kuuistisha
mkataba wake na sisi." - alisema Mkuu wa masoko wa Coca-Cola Marcelo
Pontes. |
No comments:
Post a Comment