Zikiwa zimebaki siku kadhaa mpaka
kufanyika kwa uchaguzi wa klabu ya Yanga, site hii itakuwa ikikuletea
mahojiano maalum na wagombea wa nafasi mbalimbali wanaowania uongozi
kwenye klabu hiyo kongwe ya Tanzania.
Kwa kuanzia leo tunaye
mgombea wa nafasi ya mwenyekiti Bw.Edgar William Chibula akiongelea nia
na madhumuni ya kugombea uongozi wa Yanga, pamoja na sera zake kwa
ujumla.
Jina: Edgar William Chibula Umri: 38 Utaifa: Mtanzania Elimu: Degree ya Ualimu, Amesomea ukocha chini ya ukufunzi wa Eugene Mwasamaki - pamoja na kozi ya uamuzi chini Leslie Liunda.
SABABU NA MADHUMUNI YA KUGOMBEA UONGOZI NDANI YANGA
Ikiwa utafanikiwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Yanga utaifanyia nini klabu?
"Kiukweli
jambo langu kubwa nitakalofanya kwanza ni kuifanya Yanga kuwa timu
inayojiendesha yenyewe kwa maana ya kiuchumi bila kumtegemea mtu wa
kikundi cha watu. Mpira siku hizi umekuwa biashara kubwa sana duniani na
mfano mzuri tunaona kwa vilabu vya nje ya mipaka yetu hasa barani
ulaya. Hivyo timu ikiweza kujitegemea na kujiendesha kwa faida
tutafanikiwa kufanya vitu vingi sana.
Ili kuweza kufanikisha hili
nitakaa chini na jopo la viongozi wenzangu na kuja na mipango bora ya
klabu kuitumia brand yake kufanya biashara ya bidhaa tofauti
zitakazotengenezwa kwa kutumia jina la "Yanga" ambazo ndio
kitakuwachanzo kikuu cha mapato ya klabu ambayo tayari ina utajiri wa
rasilamali watu ambao ni utitiri wa mamilioni ya watanzania wenye
mapenzi makubwa na klabu yao.
Jambo lingine kubwa ambalo
nitashughulikia ni kuunda mfumo mzuri utakaosimamia hesabu za fedha na
matumizi yake ambayo itabidi yawe wazi ili kuepeusha suala la ubadhirifu
wa fedha za klabu.
Kuunda mfumo bora wa wanachama wetu kuweza
kuchangia mawazo tofauti kupitia kwenye matawi na hatimaye yafike kwenye
uongozi wa juu na kufanyiwa kazi mara moja.
Lingine
nitakalolifanya ni kuigueza klabu kuwa kampuni itakayokuwa chini ya
wanachama Yanga. Naamini Yanga imebarikiwa na wanachama wenye ujuzi
tofauti ambao kama ungetumika vizuri Yanga inaweza kufaidika nao kuliko
kukaa klabuni na kuanza kupiga domo bila kuleta impact yoyote. Kampuni
ya Yanga itaweza pia kutoa ajira kwa wanachama wenye uwezo na
watakaokidhi matwaka na ajira zitakazotengenezwa na mwisho wa siku kila
mwanamachama wa Yanga afaidike na klabu yake na kwa upande timu yetu
ikiendelea kukua.
Nitaweka mkazo na mazingira mazuri kwa soka la
vijana nikmaanisha academy ya Yanga ambayo nitaanzisha na kuweza
kuchukua watoto wenye vipaji na kuwakuza na kwa hakika baadae
watainufaisha klabu kwa namna moja au nyngine.
Umoja - moja ya
matatizo mengi yanayoipelekea klabu yetu kushindwa kuendelea mbele ni
kukosekana kwa umoja miongoni mwa wanachama wote wa klabu hii. Kuna
makundi ambayo kiukweli mie naona ni adui wa maendelea ya klabu. Hivyo
nitahakikisha kunapatikana umoja wa wanachama wote wa Yana ambao
tutafanya kazi kwa pamoja kusukuma mbele gurudumu la maendeleo la klabu
yetu tunayoipenda kwa dhati."
KWANINI WANACHAMA WA YANGA WAKUCHAGUE WEWE NA SIO WENGINE?
Kwanza kabisa katika wanachama wenzangu wote wanaogombea uenyekiti - no offense lakini hakuna aliye na sifa kama zangu. Mimi
ni mwalimu wa soka pia ninajua mpira kuucheza na kusimamia sheria zote
za soka kwa kuwa tayari nilishasomea kozi ya ukocha na uamuzi.
Nina
uzoefu mkubwa kwenye kuongoza vilabu vya soka, kwanza nimeshawahi kuwa
mwenyekiti wa klabu ya Abajalo FC ya Dar es Salaam, na nikafanikiwa
kuiongoza kutoka kwenye ligi ya daraja la tatu mpaka la kwanza huku
tukipata mafanikio ya kubeba vikombe vingi sana. Pia niliweza kuifanya
klabu kujitegemea kwa asilimia nyingi sana kwa kubuni mipango ya
biashara ambazo ambazo kiukweli zililipa na kuifanya klabu kujitegemea.
Abajalo
chini ya Uongozi wangu iliweza kutoa wachezaji wengi wakubwa na hasa
wale waliokuja kuichezea klabu yetu ya Yanga akiwemo Kally Ongara, Ally
Mayay na wengine kibao.
Lingine nina mapenzi makubwa na klabu hii
na naamini mimi ndio mtu sahihi ambaye Yanga inahitaji. Yanga inahitaji
kuwa kiongozi ambaye atakuwa yupo full committed na kazi yake 24/7.
Yanga haihitaji kiongozi wa kutuma tu inahitaji mwenyekiti mtendaji
atakayekuwa ana-over see shughuli za kila siku za klabu. Kwenye kundi la
watu wanaoutaka uenyekiti ni mimi pekee ninayekidhi viwango hivyo." Akiwa
mmoja ya wanachama halali wa Yanga - Bwana Chibula anayo haki ya
kimsingi kugombea nafasi ya uongozi wowote kwenye uchaguzi wa klabu
hiyo. Sasa kwenye huu uchaguzi ujao wa Yanga ameamua kugombea nafasi ya
uenyekiti. Kwanini ameamua kugombea nafasi?
"Nimeamua kugombea
uenyekiti wa Yanga kwa sababu zifuatazo: Nina uwezo mkubwa kuiongoza na
kuitoa Yanga hapa ilipo na kuifanya kuwa na hadhi inayostahili kama
klabu yenye zaidi ya miaka 70. Kiukweli klabu hii imedumaa, haikuwi
kila siku hipo kama ilivyokuwa huko nyuma. Yanga imekuwa kama mtoto
mwenye ugonjwa wa upungufu wa homoni za ukuaji hivyo inashindwa kukua na
mwishowe inadumaa. Hii inatokana kupata malezi mabovu kutoka kwa wazazi
wake nikimaanisha viongozi ambao wamekuwa wakichaguliwa kuiongoza klabu
hii. Timu imekuwa ikiendeshwa kienyeji na sio kwa mfumo wa kisasa.
Viongozi hawana mipango endelevu - wamekuwa wakiendesha timu kwa mipango
ya zimamoto. Wamekuwa wakiitumia Yanga kwa manufaa yao binafsi na
kuifanya timu kubwa kama hii iendelee kutegemea vijipesa vya gate
collection. Mimi nataka kuingia kwenye uongozi wa juu niondoe hii
hali kwa sababu naamini hakuna linaloshindikana, Yanga ni mtaji tosha
hivyo kila kitu kinawezekana kufanyika kinachohitajika ni uongozi mzuri
wenye ubunifu na utakaoendesha timu kisasa. |
No comments:
Post a Comment