mashabiki wa Croatia walirusha fashfash wakati wa mechi hio mjini Poznan iliyomalizika kwa ushindi wa 3-1 jumapili iliyopita
Wahudumu wa uwanja walikabiliana na mashabiki waliovunja uzio na moja
kwa moja kwenda kumbusu Kocha wa Timu ya Taifa Slaven Bilic.
"hukumu hii imechukuliwa kwa sababu mashabiki
waliasha moto na kurusha fashifashi na mizinga pamoja na kuvamia
uwanja,imesema taarifa ya Uefa.
Wakati huo huo Uefa inachunguza madai kwamba
ndizi ilirushwa uwanjani wakati wa mechi ya kundi C kati ya Italia na
Croatia siku ya Alhamisi.
Mpiga picha mmoja alishuhudia wahudumu wa uwanja
wakiokota ndizi na kusikia miliyo ya nyani iliyoelekezwa mshambuliaji
wa Italia Mario Balotelli.
Croatia itapambana na bingwa wa Dunia na pia wa Ulaya Uhispania katika mechi ya mwisho ya makundi siku ya jumatatu mjini Gdansk.
Ushindi au sare ya 2-2 itaiwezesha Croatia kusonga mbele kujiunga na Timu nane zilizovuka hatua ya makundi.
|
No comments:
Post a Comment