Mshambulizi Cristiano Ronaldo aliwaridhisha mashabiki
wa Ureno kwa kucheza vizuri sana usiku wa Alhamisi, na juhudi zake
kuiwezesha nchi yake kuishinda Jamhuri ya Czech bao 1-0 katika mechi ya
mwanzo ya robo fainali ya Euro 2012, na kufanikiwa kuifikisha hadi nusu
fainali.
Ronaldo, ambaye alifunga magoli mawili wakati
katika mechi ya awali ya mashindano hayo nchi yako ilipocheza na
Uholanzi, aliweza kugonga mwamba katika nusu ya kwanza na ya pili katika
mechi dhidi ya Jamhuri ya Czech.
Hatimaye
aliweza kuuelekeza mpira hadi wavuni kwa kichwa, huku zikiwa zimesalia
dakika 12 kabla ya mechi kumalizika, na kipa Petr Cech akiweza kuufikia
mpira, lakini hakuweza kuuzuia kutokana na nguvu nyingi zilizotumiwa na
Ronaldo.
Ilikuwa dhahiri kwamba wachezaji wa Czech
waliingia uwanjani wakiwa na nia ya kuimarisha ngome yao, na wala sio
kushambulia, na kamwe hawakumtisha kabisa kipa wa Ureno.
Ureno sasa itakutana aidha na Uhispania au Ufaransa katika juhudi za kufuzu kwa fainali.
Bila shaka timu ambayo itakutana na Ureno
itakuwa na wasiwasi ni vipi itaweza kumzuia Ronaldo, ambaye baadhi ya
wadau wa soka wanasema kwa sasa ndiye mchezaji bora zaidi barani Ulaya
|
No comments:
Post a Comment