Mwaka 2010, mcheza soka wa kirusi Maksim
Molokoedov alikamatwa huko Santiago, Chile kwa kujaribu kuingiza kilo
sita za madawa ya kulevya aina ya Cocaine kupitia vitabu vya watoto vya
kusomea. Alihukumiwa kwenda jela miaka 3 na siku moja japokuwa akiwa
bado na mwaka mmoja wa kifungo chake , amepewa ruhusa ya kuichezea klabu
ya daraja la pili ya nchi Santiago Morning.
Akiwa chini ya
ulinzi wa walinzi wa jela, mchezaji huyo mwenye miaka 24 huwa
anafanyamazoezi na kucheza mechi mchana na jioni anarudi jela kuendelea
kutumikia adhabu yake. Kabla ya kukamatwa kwake, alikuwa akiichezea
klabu ya Pskov-74, timu ya daraja la pili nchini Urusi.
Mapenzi yake na soka yamemfanya Molokoedov ambaye ana kipaji kikubwa - kuendelea kupata special treatment huko jela. |
No comments:
Post a Comment