Shirikisho la kandanda barani Afrika, CAF, limetoa orodha ya wachezaji
34 ambao watawania tuzo ya mchezaji bora zaidi wa soka katika bara hilo
mwaka 2012.
Kati ya wachezaji hao, ni mchezaji Yaya Toure, kutoka Ivory Coast, na ambaye huichezea klabu ya Uingereza ya Manchester City.
Toure alitangazwa mshindi wa tuzo hiyo mwaka uliopita.
Katika orodha hiyo, wamo wachezaji watatu ambao huvichezea vilabu vya Afrika.
Wachezaji wawili wa Zambia, Rainford Kalaba na
Stoppila Sunzu, wote ni wachezaji wa klabu ya TP Mazembe, Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo, na Youssef Msakni kutoka Tunisia ni mchezaji wa
Esperance.
Msakni hata hivyo anatazamiwa kuihama Esperance, na kuelekea Qatar mwezi Januari mwaka ujao, kujiunga na klabu ya Lekhwiya.
Kalaba na Sunzu tayari wana sifa za kutosha,
baada ya kuwa miongoni mwa wachezaji walioiwezesha Zambia kuibuka
mabingwa katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka huu nchini
Gabon. |
No comments:
Post a Comment